Sheria Mpya nchini Kanada zinaweza kuathiri ustahiki wa dai lako la ukimbizi, hata kama tayari umewasilisha ombi lako. Baadhi ya taarifa kwenye tovuti hii zimepitwa na wakati. Tunazisasisha. Zungumza na wakili au mtoa huduma wa makazi unayemwamini. Jifunze Zaidi

Andaa Taarifa Zako

Sehemu hii inakupa muhtasari kuhusu kuandaa maelezo kwa ajili ya dai lako. Itakuambia kuhusu ushahidi muhimu wa kuunga mkono hadithi yako. Itakuelezea jinsi ya kudhibiti na kueleza maelezo yako muhimu.

Jifunze zaidi kuhusu ushahidi na nyaraka muhimu katika Sehemu ya 5: Jitayarishe kwa Usikilizaji Wako.

Andika hadithi yako

Inasaidia kuandika hadithi ya kile kilichokupata na kwa nini unaogopa kurudi katika nchi yako. Panga hadithi yako kwa mpangilio, kuanzia mwanzo hadi mwisho, na ujumuishe tarehe nyingi iwezekanavyo. Hii inaweza kukusaidia kutambua ushahidi muhimu kwa dai lako. Hakikisha umejumuisha kila jambo muhimu na usikose kueleza taarifa yoyote. IRB-RPD inaweza kukataa ikiwa utazuia maelezo au utawasilisha maelezo mapya kwenye usikilizaji wako.

Kusanya ushahidi wako

Ni muhimu kukusanya ushahidi wa kuunga mkono dai lako. Ushahidi husaidia IRB-RPD kuamini kilichotokea kwako, na kuelewa hali katika nchi yako na kwa nini huwezi kurudi.

Baadhi ya mifano ya ushahidi unoaweza kukusanya ni:

  • Nyaraka zinazothibitisha wewe ni nani
  • Ushahidi unaoonyesha kilichotokea kwako ni kweli
  • Hati au ripoti za habari zinazoonyesha jinsi nchi yako ilivyo na kwa nini uko hatarini huko
  • Barua au hati za kisheria (hati za kiapo) kutoka kwa watu wanaoweza kusema kuwa hadithi yako ni ya kweli
  • Ripoti zinazoonyesha kuwa uliuliza usaidizi kutoka kwa wakala wa serikali katika nchi yako

Jaribu kupata chochote unachohitaji kutoka nchi yako (nchi yako au mahali ulipoishi kwa muda) haraka iwezekanavyo. Kupata ripoti za polisi au hospitali kunaweza kuchukua muda mrefu. Ikiwa huwezi kupata kitu, weka rekodi ya jinsi ulivyojaribu kukipata.

Kagua hati zako na ushahidi wako

Ni muhimu kusoma ushahidi na nyaraka zako zote ili kutafuta makosa. Mtu anaweza kukuandikia barua ya usaidizi ambayo hailingani na maelezo yaliyoko katika Fomu yako ya BOC. Huenda ukahitaji kuzungumza na mwandishi huyo ili uweze kueleza kwenye usikilizaji wako. Zungumza na mwakilishi wako wa kisheria kuhusu nini cha kufanya. Ni muhimu sana kwamba IRB-RPD  waamini sehemu zote muhimu za hadithi yako.

Tafsiri hati zote

Ushahidi wote lazima utafsiriwe kwa Kiingereza au Kifaransa. Hii inachukua muda kwa hivyo ifanye haraka iwezekanavyo. Wasiliana na mwakilishi wako wa kisheria kuhusu unachohitaji kutafsiri.

Weka nakala za hati zako zote

Hifadhi nakala za hati zako zote:

  • BOC yako na fomu nyingine za uhamiaji
  • Hadithi yako
  • Ushahidi wote, maombi yote na barua zote ambazo wewe au mwakilishi wako wa kisheria mutapeana kwa  IRB, CBSA au IRCC.
  • Barua, hati, au notisi zozote za miadi ambazo IRB, CBSA, au IRCC itakutumia

Pata faili ya kuweka hati zako salama na kuzipanga. Weka hati zako hadi uwe raia wa Kanada.

Weka anwani yako sahihi

Hakikisha anwani yako ni sahihi kila wakati. Hii ni muhimu ili usikose taarifa yoyote kuhusu dai lako.