Mikutano ya kusikiliza maombi ya wakimbizi ni ya faragha na hayaruhusu umma kuhudhuria. Ni watu fulani pekee wanaweza kuhudhuria kikao chako cha ombi la mkimbizi:
Mwanachama wa IRB-RPD
Mtoa-uamuzi katika kikao chako anaitwa Mwanachama. Mwanachama wa IRB-RPD anaendesha kesi na anaamua kukubali au kukataa dai lako. Mwanachama anatarajiwa kukuongolesha kwa heshima na uangalifu. Mwanachama atasoma Fomu yako ya BOC na ataangalia ushahidi wako wote kabla na mkutano kuanza. Atakuuliza maswali wakati wa kusikilizwa kwako ili kumsaidia kufanya uamuzi kuhusu dai lako la ukimbizi.
Mwakilishi wa kisheria
Mwakilishi wako wa kisheria anaweza kuwa wakili, mshauri wa uhamiaji, au mwakilishi wa kujitolea. Katika jimbo la Quebec, Mthibitishaji wa umma anaweza kukuwakilisha, na katika jimbo la Ontario, mwanasheria anaweza kukuwakilisha.
Wakati Mwanachama anakuuliza maswali, mwakilishi wako wa kisheria anaweza kukuelezea ni nini anamaanisha. Mwakilishi wako wa kisheria hawezi kukujibia maswali. Lazima uwe tayari kumjibu Mwanachama mwenyewe. Mwakilishi wako wa kisheria atakuwa na nafasi ya kukuuliza maswali, lakini kwa kawaida, lazima asubiri mpaka Mwanachama amalize kukuuliza maswali kwanza.
Mwishoni mwa kusikilizwa kwako, mwakilishi wako wa kisheria anaweza kutoa muhtasari wa dai lako kwa Mwanachama. Hii inaitwa mawasilisho. Mawasilisho yanaweza kufanywa kwa kumuambia Mwanachama kwenye kikao cha kusikilizwa, au yanaweza kuandikwa kwenye barua na mwakilishi wako wa kisheria na kutumwa kwa IRB-RPD baada ya kusikilizwa kwako.
Wakili wa Waziri
Wakili wa Waziri ni mfanyakazi wa CBSA au IRCC. Wakili wa Waziri hahusiki katika madai ya kila mtu ya ukimbizi. Watahusika ikiwa wanataka kupinga dhidi ya dai lako la ukimbizi. Ikiwa Wakili wa Waziri anahusika, ni kwa sababu wana wasiwasi:
- kuhusu wewe ni nani au kuhusu hati zako,
- kwamba hujasema ukweli, au
- kwamba wewe ni mhalifu au wewe ni mwanachama wa shirika la kigaidi.
Utajulishwa kama Wakili wa Waziri atahusika katika madai yako. Kabla ya kusikilizwa, Wakili wa Waziri atakutumia wewe au mwakilishi wako wa kisheria Notisi ya Kuingilia kati. Katika notisi, wanaelezea jinsi watahusika na kwa nini watahusika. Notisi itasema kama watakuja kwenye kusikilizwa kwako au kama watatuma hati tu. Unapaswa kupata notisi angalau siku kumi au zaidi kabla ya kusikilizwa kwako. Isome kwa makini na uwe tayari kuizungumzia. Ikiwa Wakili wa Waziri yuko kwenye kikao chako, kuna uwezekano atakuuliza maswali.
Mkalimani
Jukumu la mkalimani ni kuhakikisha kwamba kila mtu anamuelewe mwengine vizuri. Hata kama unajua Kiingereza au Kifaransa, ni vizuri kuwa na mkalimani ili kuepuka makosa. Wakalimani wa IRB hawatatoa habari zozote kukuhusu au kuhusu dai lako kwa mtu yeyote asiyehusika katika mkutano huo.
IRB-RPD itakupatia mkalimani mtaalamu bila malipo kwako anayejua lugha na lahaja yako. Ikiwa hukusema kuwa unataka mkalimani katika fomu yako ya BOC, bado unaweza kumuitisha. Andika kwa IRB-RPD siku kumi au zaidi kabla ya kusikilizwa kwako ili kuomba upewe mkalimani.
Unaweza kuomba mkalimani wa jinsia mahususi au wa jinsia sawa na wewe ikiwa ungejisikia vizuri zaidi na hili. Kwa mfano, kama dai lako la ukimbizi linatokana na jambo nyeti lililokutokea na utaona ni rahisi kuwa na mkalimani ambaye ni jinsia sawa na wewe, wajulishe IRB-RPD.
Mashahidi
Unaweza kuwa na mashahidi katika kusikilizwa kwako watakao zungumza kuhusu madai yako. Shahidi ni mtu ambaye anaweza kuthibitisha kilichotokea kwako. Mashahidi wanaweza kuwa ndani ya Kanada au katika nchi nyingine. Shahidi pia anaweza kuwa mtu mwenye utaalamu kuhusu masuala yanayohusiana na dai lako la ukimbizi.
Chagua mashahidi wako kwa uangalifu ukitumia usaidizi wa mwakilishi wako wa kisheria. Hakikisha unawatayarisha mashahidi kabla ya kusikilizwa kwako. Wajulishe mashahidi wako kwamba watachosema lazima kiwe cha kweli. Iwapo ungependa kualika mashahidi kwenye kikao chako, wewe au mwakilishi wako wa kisheria, ni lazima muandike kwa IRB-RPD (na pia kwa Wakili wa Waziri ikibidi) siku kumi au zaidi kabla ya kusikilizwa kwako. Wape:
- Jina la shahidi wako
- Taarifa fupi ikieleza kwa nini wanazungumza
- Uhusiano wako na shahidi
- Unadhani wataongea kwa mda gani
Watazamaji
Unaweza kualika mtazamaji mmoja au zaidi kwenye kikao chako cha mkimbizi kama itakusaidia ujiskie vizuri. Mtazamaji anaweza kuwa rafiki, jamaa, au mtu wa jumuiya yako.
Katika kusikilizwa kwako, Mjumbe atawauliza watazamaji wajitambulishe. Wakati wa kusikilizwa, watazamaji hawaruhusiwi kuzungumza na lazima watulie. Mtazamaji hawawezi pia kuwa shahidi.
Watoto wako wenye umri wa miaka 18 au chini
Ikiwa una watoto walio na umri wa miaka 18 au zaidi, lazima waje kwenye kikao cha kusikilizwa kwa wakimbizi. Watoto walio chini ya umri wa miaka 18 si lazima waende kwenye kikao hicho isipokuwa ikiwa Mwanachama amewaita. Kwa usikilizaji wa mtandaoni, hakikisha kuwa kuna mtu atakaye wangalia watoto wako wadogo kando na mahali ulipo. Unaweza kuwa unazungumzia matukio mabaya. Haya ni mambo ambayo huenda hutaki watoto wako wayasikie. Ikiwezekana, waambie watoto wako waende shuleni au wakae na jamaa au marafiki, au mlipe mtu awaangalie.
Mwakilishi Mteule
IRB-RPD humtaja Mwakilishi Aliyeteuliwa kuwawakilisha watoto wadogo au watu wazima ambao hawawezi kuelewa mchakato wa ukimbizi. Mwakilishi Aliyeteuliwa humsaidia mtu huyo kuelewa kinachotokea na kumsaidia kuunda kesi bora zaidi. Mwakilishi Mteule anaweza kuulizwa maswali wakati wa kusikilizwa. IRB-RPD kwa kawaida huchagua mzazi kama Mwakilishi Aliyeteuliwa ikiwa dai la mtoto limeunganishwa na dai la mzazi wake.
