Ziara ya Matayarisho (Ready Tours)
Je, unashangaa jinsi gani unaweza kujiandaa kwa ajili ya kusikilizwa kwa ukimbizi wako? Je, unajiuliza jinsi ya kukata rufaa iwapo dai lako la ukimbizi limekataliwa? Hudhuria Ziara ya Matayarisho.
Kuhusu Ziara ya Matayarisho
Ziara ya Matayisho, ni warsha pepe zisizolipishwa ambapo wadai wakimbizi hujitayarisha kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi zao za ukimbizi na kujifunza kuhusu mchakato wa rufaa ya ukimbizi.
Hudhuria Ziara ya Matayarisho ili kujifunza kuhusu mchakato wa kusikilizwa hearing kwa wakimbizi na kukata rufaa appeal kutoka kwa mtu anayefanya kazi katika Bodi ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Kanada (IRB). Uliza maswali yako, ungana na wengine, na ujifunze jinsi ya kujiandaa!

Ziara ya Matayarisho ya Rufaa (Appeal Ready Tours)
- Jifunze jinsi ya kutayarisha na kuwasilisha rufaa ukipata uamuzi usiofaa
- Kwa wakata rufaa ambao wamepokea uamuzi mbaya
- Kwa wadai wakimbizi wanaosubiri kusikilizwa au uamuzi wao
- Wakalimani wanapatikana
- Wafanyakazi wa jamii au makazi wanahimizwa kuhudhuria
Jinsi ya kuchukua Ziara ya Matayarisho
- Jisajili mtandaoni
- Chagua lugha yako (mkalimani bila malipo ametolewa)
- Pata barua pepe ili kuthibitisha kuwa umejiandikisha
- Pata kiungo cha Microsoft Teams kwa Ziara ya Matayarisho
- jiunge na Ziara ya Matayarisho kwenye kompyuta, kompyuta kibao au simu!

