Ziara ya Kujitayarisha Kusikilizwa (Hearing Ready Tour)

Ziara ya Kujitayarisha Kusikilizwa ya wakimbizi huelimisha wadai wa ukimbizi na kuwasaidia kujitayarisha kwa ajili ya kusikilizwa kwa dai lao. Ikiwa wewe ni mdai wa ukimbizi, unaweza kujiandikisha ufanye Ziara ya mtandaoni ya Kujitayarisha Kusikizwa kwa dai lako bila malipo yoyote kutoka sehemu yoyote nchini Kanada. Wakala wa wageni au wafanyakazi wa kijamii pia wanaweza kuhudhuria ziara hii.

Jisajili ili uhudhurie Ziara ya Kujitayarisha Kusikilizwa

Ninajiandikisha kama…

Je, uko Kanada sasa?

Je, umetoa madai ya ukimbizi?

Ziara ya Kujitayarisha hufanywa kwa lugha ya Kiingereza na Kifaransa.
Je, unahitaji mkalimani ili ufanye ziara kwa lugha nyingine?

Chagua lugha utakayopendelea kuitumia kwenye Ziara hii ya Kujitayarisha.

Chagua lugha unayohitaji kutafsiriwa wakati unafanya Ziara ya Kujitayarisha.

Taja lugha unayopendelea.

Ni lazima uwe nchini Kanada na uwe umepata hati ya mdai wa ulinzi wa mkimbizi (IMM1442) ili uweze kushiriki katika Ziara ya Kujitayarisha kusikilizwa. Soma maswali yanayoulizwa mara kwa mara ili upate maelezo zaidi. Tafadhali rudi kwenye tovuti hii na ujisajili ikiwa utagundua kuwa unastahiki. Asante.

Je, ungependa kufanya ziara gani ya Kujitayarisha Kusikizwa?


Tarehe za Ziara ya Kujitayarisha Kusikizwa Zinazokuja

Chagua Ziara ya mtandaoni ya Kujitayarisha Kusikizwa ambayo inakufaa. Unaweza kuhudhuria popote ulipo nchini Kanada. Saa iliyotajwa hapa ni kulingana na majira ya Pasifiki – rekebisha masaa kulingana na eneo lako.

Kizungu pekee

  • Machi 31, 2026
    10:30 mu – 12:30 um (PST)
  • Aprili 14, 2026
    10:30 mu – 12:30 um (PST)

Kifaransa pekee

  • Aprili 2, 2026
    10:30 mu – 12:30 um (PST)

Kizungu na lugha nyingine

  • Aprili 2, 2026
    9:30 mu – 11:30 mu (PST)
  • Aprili 17, 2026
    9:30 mu – 12:30 um (PST)

Ziara ya Kujitayarisha Kusikizwa hukupa fursa ya:

  • Kuelewa kitakachotokea siku ya kusikilizwa kwako
  • Kujifunza jinsi ya kujiandaa kwa ajili ya kusikilizwa kwa ombi lako mtandaoni.
  • Jifunze jinsi ya kuwasilisha ushahidi
  • Gundua ni nani anayeweza kuhudhuria kikao chako cha mkimbizi
  • Kutana na mfanyakazi wa Kamati ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Kanada (IRB)
  • Uliza maswali yako.

Wadai wa ukimbizi wanasema nini kuhusu Ziara ya Kujitayarisha Kusikizwa

Kila mdai wa ukimbizi ahakikishe amehudhuria Ziara ya Kujitayarisha! Natamani ningejua mapema kuhusu ziara hii ya kujitayarisha.

Kitu muhimu zaidi kuhusu Ziara hii ya Kujitayarisha ya mtandaoni ni kwamba utapata kujua jinsi usikilizaji wa wakimbizi unavyofanyika na nini cha kutarajia.

Ilisaidia sana na ni fursa nzuri ya kupata nafasi ya kuuliza maswali kuhusu mchakato wa kusikilizwa kwa wakimbizi na kupata majibu mazuri na ya kuelimisha.

Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara

Ndiyo, kama huwezi kufanya ziara kwa lugha ya Kiingereza au Kifaransa, unaweza kuomba upate mkalimani. Tutakupa mkalimani bila malipo. Unapojaza fomu ya usajili, bonyeza “Ndiyo” sehemu inayouliza “Je, unahitaji mkalimani ili ufanye ziara kwa lugha nyingine?” Halafu chagua lugha utakayoipendelea.

Ndiyo, unahitajika uwe nchini Kanada ili uweze kuhudhuria Ziara ya Kujitayarisha. Ziara hizi ni za watu ambao wameshawasilisha dai la ukimbizi nchini Kanada, na wanasubiri dai lao lisikizwe na Kamati ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Kanada (IRB).

Ziara ya Kujitayarisha Kusikizwa hufanyika kila baada ya wiki 2-4. Ziara za Kiingereza pekee na za Kifaransa pekee hufanyika mara moja kila mwezi. Ziara za Kujitayarisha za Lugha nyingine zinazohitaji mkalimani hufanyika kila baada ya wiki mbili. Wakati unajaza fomu yako ya usajili utaweza kuchagua tarehe ambayo itakufaa zaidi.

Ziara ya Kujitayarisha hufanywa mtandaoni. Huhitaji kwenda ofisi yoyote au mahali maalum pa kuhudhuria. Ziara ya Kujitayarisha hufanyika kwenye tovuti ya Teams. Utatumiwa barua pepe yenye tovuti utakayotumia kujiunga kwenye ziara mtandaoni pamoja na maagizo ya jinsi ya kujiunga kabla ya mda wa Ziara hiyo kuwasili.

Je, umepata Ugumu wowote wakati wa kujiandikisha kuhudhuria Ziara ya Kujitayarisha?

Wasiliana na [email protected]