Karibu kwa Dai Langu la Ukimbizi ( My Refugee Claim)
Dai Langu la Ukimbizi ni la watu wanaodai ukimbizi nchini Kanada.
Dai Langu la Ukimbizi linatoa nyenzo tatu – tovuti hii, Kijitabu cha Mwelekeo (Orientation Booklet), na Ziara ya Matayarisho (Ready Tours) – ili kukusaidia kupata taarifa, kuunganishwa, na kujiandaa katika safari yako yote ya kudai ukimbizi.
Jinsi ya kutumia tovuti hii
Safari yako kupitia mchakato wa ulinzi wa wakimbizi wa Kanada itakuwa yako mwenyewe. Lakini kuna hatua muhimu ambazo wadai wakimbizi wote lazima wachukue. Tumia sehemu nane za tovuti hii ili kupata mahali ulipo katika mchakato huo, jifunze unachopaswa kufanya, na ujitayarishe kwa yatakayofuata.

Kijitabu cha Mwelekeo (Orientation Booklet)
Tazama na uchapishe Kijitabu cha Mwelekeo. Nyenzo hii ya vitendo inakupa muhtasari wa mchakato wa ulinzi wa wakimbizi wa Kanada. Itumie unaposonga mbele katika safari yako.
