Kusikilizwa kwa dai lako la ukimbizi ndio sehemu muhimu zaidi ya huu mchakato. Wakati wa kusikilizwa kwako, au baada ya kusikilizwa kwako, utagundua kama dai lako la ukimbizi limekubaliwa au limekataliwa.
Mkutano wa kusikilizwa dai lako ni fursa yako ya kusimulia hadithi yako na kueleza ni kwa nini unahitaji ulinzi wa Kanada. Huu mkutano ni wa faragha na ni salama.
Wakati wa mkutano wa kusikiliza ombi lako unaweza kujisikia ni kama uko mahakamani lakini sio hivyo. Wanaofanya maamuzi wanaitwa Wanachama na wamepewa mafunzo maalum ya kuamua madai ya ukimbizi. Mwanachama ataamua dai lako kwa haki.
Mikutano ya kusikiliza wakimbizi kwa kawaida huchukua muda wa masaa 3-4, lakini unaeza kuwa mrefu au mfupi zaidi kulingana na mambo yatakavyokwenda. Mikutano hii mara nyingi hufanywa mtandaoni, ila mengine yanafanyika ana kwa ana katika ofisi ya IRB.
