Kipindi cha Kusubiri

Sehemu hii inakupa mawazo muhimu kuhusu jinsi ya kutumia muda wako vizuri, hasa unaposubiri kusikilizwa kwa dai lako la ukimbizi.

Kuwa na subra

Kusubiri ni sehemu ya kawaida ya kufanya madai ya ukimbizi. Huenda ukalazimika kusubiri kusikilizwa kwa dai lako au kusubiri ili kujua ikiwa dai lako litakubaliwa.

Jitayarishe

Tumia muda wa kusubiri ili kujiandaa kwa ajili ya kusikilizwa kwako:

  • Hudhuria Ziara ya Kujitayarisha Kusikizwa ya IRB-RPD. Utajifunza jinsi ya kujiandaa kwa mkutano wako wa kusikilizwa na kile kitakachotokea wakati wa kusikilizwa. Pia utapata kukutana na wafanyakazi wa IRB na kuuliza maswali kuhusu kusikilizwa
  • Pitia fomu yako ya BOC, simulizi yako pamoja na ushahidi uliotuma.
  • Tafuta maelezo yoyote ambayo hayalingani katika fomu yako ya BOC, hadithi yako, madokezo ya mahojiano, ushahidi na hati nyingine (pamoja na maombi ya visa ya ng’ambo). Mwambie mwakilishi wako wa kisheria. Unaweza kutaka kutuma mabadiliko kwa IRB-RPD.
  • Endelea kufuatilia habari kutoka kwa nchi yako. Jambo likitokea ambalo linahusiana na dai lako, mwambie mwakilishi wako wa kisheria.

Anza maisha upya

Tumia wakati huu wa kungojea kuanza maisha yako na ya familia yako. Unaweza:

  • Boresha Kiingereza chako au Kifaransa
  • Kupata kazi
  • Endelea kufanya mazoezi
  • Jitolee katika jamii
  • Jiunge na kundi la wageni nchini
  • Wajue majirani zako

Sehemu inayofuata ya mwongozo: 2.5 Pata Usaidizi Unaohitaji