Mahitaji ya ushahidi
Ushahidi wako wote lazima uwe kwa lugha ya Kiingereza au Kifaransa. Ikiwa una hati katika lugha nyingine, unahitaji kuzitafsiri kwa Kiingereza au Kifaransa. Ikiwa unawasilisha video au sauti iliyorekodiwa kama ushahidi, utahitaji uandike nakala inayohadithia ya kila kinachosemwa. Nakala hii lazima pia itafsiriwe kwa Kiingereza au Kifaransa.
Kuna tarehe ya makataa ya kutuma ushahidi wako. Ushahidi wote lazima utumwe kwa IRB-RPD angalau siku 10 kabla ya kusikilizwa kwa ombi lako la mkimbizi. Hakikisha umetuma ushahidi wako kabla ya mda wa kutuma ushahidi kuisha.
Ushahidi lazima uwasilishwe katika muundo maalum. Endelea kusoma hapa chini ili ujue zaidi:
Ikiwa una mwakilishi wa kisheria
Ikiwa una mwakilishi wa kisheria, atawasilisha nyaraka zako kwa niaba yako. Mpe mwakilishi wako wa kisheria ushahidi na nyaraka zako zote. Anaweza kukusaidia kuamua ni nyaraka zipi ni muhimu na ataziwasilisha kwa IRB-RPD. Hakikisha unampa muda wa kutosha.
Ikiwa huna mwakilishi wa kisheria
Ikiwa umealikwa kutumia My Case, lazima uwasilishe ushahidi wako kupitia tovuti ya My Case portal. Unaweza kutumia njia nyingine tu ikiwa utapata ruhusa kutoka kwa IRB-RPD.
Ikiwa unajiwakilisha mwenyewe na hujapokea mwaliko wa My Case, unaweza kuendelea kutuma nyaraka kwa barua pepe (inapendekezwa) au kwa posta.
Unapowasilisha ushahidi wako, kumbuka mambo muhimu yafuatayo:
- Hakikisha hati zako zote ziko kwenye karatasi ya ukubwa wa 8.5 x 11. Hati zilizoandikwa lazima ziwe na herufi zilizo na ukubwa wa angalau 12.
- Weka hati zako pamoja na uziandike namba kutoka ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho.
- Tengeza ukurasa wa jalada wenye jina na anwani yako, tarehe, nambari yako ya faili ya IRB-RPD, orodha ya hati zako zote, na nambari zao za ukurasa.
- Tengeneza nakala za hati zako zote. Weka nakala ya asili
- Ikiwa unawasilisha hati zako kwa kutumia barua pepe hakikisha kuwa ziko katika umbizo la PDF
Tuma nakala moja ya kifurushi chako cha hati kwa IRB-RPD katika eneo lako. Eneo ulilopo linategemea na mahali unapoishi. Ukihamia eneo lingine, unaweza kuomba dai lako lihamishwe hadi eneo hilo:
Ikiwa unaishi British Columbia, Alberta, Saskatchewan, Manitoba, Yukon, Northwest Territories.
Barua pepe
- [email protected]
- Fuata maelekezo haya kwa makini: Lazima utume nyaraka zako kama viambatisho katika mfumo wa PDF. Faili za PDF hazipaswi kuzidi 20MB. Katika mstari wa mada, weka nambari yako ya UCI (na nambari yako ya IRB-RPD na tarehe ya usikilizaji ikiwa unayo) na eleza kuwa nyaraka za ushahidi zimeambatishwa. Usiandike chochote katika mwili wa barua pepe.
Barua
Ikiwa huwezi kutumia njia nyingine zozote, unaweza kutumia huduma ya posta au courier. Hifadhi nyaraka zako za asili na risiti. Hakikisha unatuma kifurushi chako mapema ili kifike kwa wakati.
- IRB-RPD, Minto Place, Canada Building 344 Slater Street, Ghorofa ya 12 Ottawa, Ontario Canada, K1A 0K1I
Ana kwa ana
- IRB–RPD, 300 West Georgia Street, Suite 1600 Vancouver, BC V6B 6C9
- Ikiwa unaishi Vancouver unaweza kuwasilisha hati zako mwenyewe katika ofisi ya IRB.
Ikiwa unaishi Ontario (isipokuwa Ottawa na Kingston)
Barua pepe
- [email protected]
- Fuata maagizo haya kwa uangalifu: Lazima utume hati zako katika umbizo la PDF. Faili za PDF haziwezi kuwa na ukubwa uliozidi MB 20. Katika mstari wa mada, weka nambari yako ya UCI (na nambari yako ya IRB-RPD na tarehe ya kusikilizwa ikiwa unayo) pamoja na kutaja ni hati gani unazozituma. Usiandike chochote kwenye mwili wa barua pepe.
Barua
Ikiwa huwezi kutumia njia nyingine zozote, unaweza kutumia huduma ya posta au courier. Hifadhi nyaraka zako za asili na risiti. Hakikisha unatuma kifurushi chako mapema ili kifike kwa wakati.
- IRB-RPD, Minto Place, Canada Building 344 Slater Street, Ghorofa ya 12 Ottawa, Ontario Canada, K1A 0K1
Ana kwa ana
- 25 St. Clair Avenue East, Suite 400, Toronto, Ontario M4T 0A8
- Ikiwa unaishi Toronto unaweza kuwasilisha hati zako mwenyewe katika ofisi ya IRB.
Ikiwa unaishi Quebec, New Brunswick, Nova Scotia, Prince Edward Island, Newfoundland, Nunavut, Kingston (Ontario), Ottawa (Ontario)
Barua pepe
- [email protected]
- Fuata maagizo haya kwa uangalifu: Lazima utume hati zako katika umbizo la PDF. Faili za PDF haziwezi kuwa na ukubwa uliozidi MB 20. Katika mstari wa mada, weka nambari yako ya UCI (na nambari yako ya IRB-RPD na tarehe ya kusikilizwa ikiwa unayo) pamoja na kutaja ni hati gani unazozituma. Usiandike chochote kwenye mwili wa barua pepe.
Barua
Ikiwa huwezi kutumia njia nyingine zozote, unaweza kutumia huduma ya posta au courier. Hifadhi nyaraka zako za asili na risiti. Hakikisha unatuma kifurushi chako mapema ili kifike kwa wakati.
- IRB-RPD, Minto Place, Canada Building 344 Slater Street, Ghorofa ya 12 Ottawa, Ontario Canada, K1A 0K1
Ana kwa ana
- Guy-Favreau Complex, 200 René-Lévesque Blvd. West, East Tower, Room 102, Montréal, Quebec H2Z 1X4
- Ikiwa unaishi Montreal unaweza kuwasilisha hati zako mwenyewe katika ofisi ya IRB.