Unaweza kutuma ombi la ukazi wa kudumu (PR) nchini Kanada ikiwa IRB-RPD au IRB-RAD itakubali dai lako peke yake.
Ni muhimu kukumbuka kwamba mchakato wa ombi la makazi ya kudumu au PR unaweza kuchukua muda mrefu. Wakati wa kujibiwa kwa ombi ni tofauti kwa kila mtu. Hili ni jambo la kawaida.
Anza ombi lako
Unaweza kutuma ombi lako kwenye mtandao kutumia Tovuti ya Makazi ya Kudumu au kwa kutuma barua.
Jinsi ya kuanza ombi lako kwenye Tovuti ya Makazi ya Kudumu au PR
- Tengeza akaunti yako
- Ingia kwenye akaunti yako
- Chagua haya yafuatayo kwenye orodha itakayofuata:
- Mpango unaotumia kutuma ombi: “Makazi ya Kudumu, pamoja na Makazi Mapya ya Wakimbizi”.
- Mpango ambao unataka kuomba (2): “Mkimbizi”.
- Kitengo ambacho unatuma ombi lako: Nchini Kanada – “Mtu Aliyelindwa”.
- Jaza maelezo yako kwenye wasifu wako halafu ujaze wasifu wa familia yako.
- Bonyeza “Hifadhi na Endelea”.
Tayarisha hati zako
Ili kutuma ombi, lazima uandae:
- Orodha ya hati zinazohitajika (IMM 5286 E)
- Fomu ya Kawaida ya Kutuma Ombi ya Kanada (IMM 0008)
- Watu wanaokutegemea/Maelezo ya Ziada (IMM 0008DEP-E)
- Watu Waliolindwa na Wakimbizi wa Mkataba wa Wakimbizi (IMM 0008: Schedule 14)
- Historia yako/Habari za Ziada (IMM 5669 E : Schedule A)
- Maelezo ya Ziada ya Familia (IMM 5406 E)
- Matumizi ya Mwakilishi (IMM 5476 E)
- Nakala ya Taarifa ya Uamuzi ambayo yakupa hadhi ya Mkimbizi wa Mkataba au Mtu Aliyelindwa nchini Kanada
- Picha moja ya pande mbili ya dijitali iliyopigwa hivi majuzi (picha ya pasipoti iliyopigwa muhuri nyuma na duka la kupiga picha)
- Nakala za hati zako za kitambulisho ambazo zilichukuliwa kutoka kwako:
- pasipoti (hata kama muda wake umeisha),
- Hati za usafiri,
- cheti cha kuzaliwa kilichotafsiriwa, na
- hati nyingine zozote za utambulisho kama vile cheti cha ndoa kilichotafsiriwa.
Watu wanaokutegemea na watu wa familia yako
Kama una watu wanaokutegemea ndani au nje ya Kanada, lazima ujaze fomu tofauti za kila mmoja wao. Lazima utayarishe:
- Orodha ya Hati Zinazohitajika (IMM 5286 E)
- Fomu ya Kawaida ya Maombi ya Kanada (IMM 0008 E)
- Watu Waliolindwa na Wakimbizi wa Mkataba wa Geneva (IMM 0008: Schedule 14)
- Historia yako/Habari za kujitolea (IMM 5669 E : Schedule A)
- Maelezo ya ziada ya familia yako (IMM 5406 E)
- Matumizi ya Mwakilishi (IMM 5476 E), kama ulitumia mwakilishi
- Picha moja ya pande mbili ya dijitali (picha ya pasipoti)
- Nakala za pasipoti zao, hati za kusafiria, au hati za kitambulisho
- Nakala za hati zinazothibitisha jinsi munavyohusiana, kama vile vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya ndoa, au vyeti vya kuthibitisha ndoa isiyo rasmi (Fomu 5409)
Katika ombi lako, lazima uwajulishe IRCC iwapo una mume au mke au jamaa yoyote anayekutegemea uliyempata baada ya kuwasili katika nchi ya Kanada.
Huenda usijue mahali baadhi ya watu wa familia yako walipo, lakini bado unaweza kuwaorodhesha katika ombi lako. Ukipata makazi ya kudumu au PR, watakuwa na muda wa mwaka mmoja ili kutuma maombi yao ya makazi ya kudumu. Mtu ambaye IRCC inamchukulia kuwa mwana familia yako pekee ndiye anayeweza kufanya hivi. Watu ambao unawachukulia kama familia lakini si ndugu wa asili hawawezi kufanya hivi. Ongea na wakili ikiwa una jamaa ambao si ndugu wa damu.
Tafsiri hati zako
Ikiwa una hati yoyote (pamoja na mihuri yoyote) ambayo haijaandikwa kwa lugha ya Kiingereza au Kifaransa, lazima utume:
- Tafsiri ya Kiingereza au Kifaransa. Tazama tovuti ya IRCC ili ufuate mahitaji yao ya kutafsiri hati.
- Ikiwa huwezi kupata mtafsiri aliyeidhinishwa atafsiri hati zako za kitambulisho, unaweza kutumia mfasiri ambaye hajaidhinishwa. Ikiwa utafanya hivi utahitaji:
- hati ya kiapo kutoka kwa mtu aliyefanya tafsiri hiyo, na
- nakala ya hati asili iliyothibitishwa. Ni lazima iwe imethibitishwa nchini Kanada na mthibitishaji rasmi, kamishna wa viapo, au kamishna wa kuapisha watu viapo.
Lipa ada
Ni lazima ulipe ada ukiwa unatuma ombi lako au la familia yako la makazi ya kudumu (PR). Utalipa ada kwenye mtandao. Ili kulipa ada mtandaoni utahitaji:
- Barua pepe ya kufungua akaunti yako pamoja na neno la siri
- Uwepo wa kompyuta ili uhifadhi risiti yako
- Uwepo wa mashine ya kuchapa picha (ili uweze kuchapisha risiti), na
- Kadi ya Mkopo, au Kadi ya benki ya Mastercard, au ya Visa.
Ukiwa uko tayari kulipa:
- Nenda kwa sehemu ya Malipo ya Mtandaoni.
- Fuata maagizo yote
- Ukifika mwisho, bofya sehemu ya kuchapisha risiti rasmi ya IRCC iliyo na msimbo upau.
- Tengeneza chapa mbili
- Hifadhi nakala moja kwenye kompyuta yako.
- Jitumie nakala moja kwenye barua yako ya pepe
- Weka nakala ya risiti hii uliyochapisha pamoja na maombi yako.
- Hifadhi nakala za risiti zitakazobakia kwenye rekodi zako.
Alama za vidole
Ikiwa utahitaji kutuma alama za vidole, baada ya kutuma ombi la kuwa mkazi wa kudumu na kulipa ada za kuchukuliwa alama za vidole, utatumiwa Barua ya Masharti ya Kuchukuliwa Alama za Vidole (BIL). Barua hii itakujulisha kwamba muda umefika wa kwenda kuchukuliwa alama za vidole. Pia, barua hii itakuwa na tovuti ya sehemu za ofisi za Huduma za Kanada ambapo utaweza kwenda kuchukuliwa alama zako za vidole ndani ya nchi ya Kanada pamoja na nje ya nchi.
Nenda uchukuliwe alama zako za vidole haraka iwezekanavyo. Ombi lako halitaenda mbele mpaka alama zako za vidole zitumwe.
Tuma ombi lako
Unaweza kutuma ombi lako na kutuma fomu zako kupitia Tovuti ya Makazi ya Kudumu.
Unaweza pia kutuma ombi lako la karatasi kwa IRCC kwa kuwatumia barua:
Anwani ya barua
Protected Persons in Canada application Box 12153 STN A Sydney, NS B1P 0L1
Anwani ya barua
Protected Persons in Canada application 3050 Wilson Avenue New Waterford, NS B1H 5V8
Hatua za mwisho
Iwapo utawasilisha taarifa na hati zinazohitajika kama ipasavyo kwenye ombi lako la madai ya ukazi wa kudumu (PR), utapokea barua kutoka kwa IRCC ambayo itakuambia ikiwa umekubaliwa kuwa mkazi wa kudumu au la.
Kitambulisho chako cha PR kitatumwa kwenye barua. Ni muhimu kuhakikisha kwamba IRCC wana anwani yako ya sahihi ili uipate barua hii!
Wakati mwingine, IRCC itataka kukuhoji. Huenda wakataka uthibitishe ukweli wa maelezo au uwatumie maelezo zaidi. Baada ya IRCC kupata kile wanachohitaji, utaweza kupata jibu la ombi lako la makazi ya kudumu (PR) katika mahojiano yako ya mwisho.
