Ikiwa IRB-RPD itakataa dai lako, inaweza kuwa kwa sababu:
- Hawaamini dai lako.
- Hawaamini kuwa unasema ukweli kuhusu wewe ni nani
- Hawafikirii una sababu nzuri za kuhitaji ulinzi.
- Wanafikiri mamlaka ya nchi yako yanaweza kukulinda.
- Wanafikiri kuwa kuna sehemu katika nchi yako ambayo ni salama kwako kuishi na inakufaa.
- Wewe ni raia au mkazi wa kudumu wa nchi nyingine ambapo hakuna hatari yoyote.
- Umehusika katika uhalifu mkubwa, uhalifu wa kivita, au uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Unachoweza kufanya baada ya dai lako kukataliwa
Dai lako likikataliwa, bado kuna njia za kubakia nchini au kuwa mkazi wa kudumu nchini Kanada. Unaweza ku:
- Tuma Rufaa kwa Tume ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Kanada – Kitengo cha Rufaa ya Wakimbizi (IRB-RAD)
- Tuma ombi kwa Mahakama ya Shirikisho la Kanada kwa Marudio ya Kimahakama
- Ombi la Kupima Hatari ya Kuondolewa Kabla ya Kuondolewa nchini (PRRA)
- Omba makazi ya kudumu kwa misingi ya Kibinadamu na Huruma (H&C)
