Sheria Mpya nchini Kanada zinaweza kuathiri ustahiki wa dai lako la ukimbizi, hata kama tayari umewasilisha ombi lako. Baadhi ya taarifa kwenye tovuti hii zimepitwa na wakati. Tunazisasisha. Zungumza na wakili au mtoa huduma wa makazi unayemwamini. Jifunze Zaidi

Pata Uamuzi Wako

Kamati ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Kanada – Kitengo cha Ulinzi wa Wakimbizi (IRB-RPD) huwa ndio wanaamua kama dai lako la ukimbizi litakubaliwa nchini Kanada.

Baada ya dai lako la ukimbizi kusikilizwa, Mjumbe wa Kamati anaweza:

  • Kukwambia kwamba kesi yako itahitaji kuendelea baadaye.
  • Kukujulisha kama dai lako limekubaliwa au kukataliwa. Huu unaitwa uamuzi wa matamshi.
  • Atakuambia kwamba uamuzi utatumwa kwako au kwa mwakilishi wako wa kisheria baada ya usikilizaji. Hii inaitwa uamuzi ulioandikwa.
  • Wanaweza pia kukupa muda zaidi wa kutuma hati za ziada au maelezo ya ziada kabla hawajatoa uamuzi wao.