Ikiwa huna uzoefu wa kuzungumza kwa Kiingereza au Kifaransa unaweza kuhitaji mkalimani wa kukusaidia kuwasiliana wa watu. Ni muhimu kuwa na mkalimani ili uelewe kile kinachotokea wakati wa dai lako la ukimbizi. Baadhi ya mifano ya wakati unaweza kuhitaji mkalimani ni:
- Wakati unakutana na mwakilishi wako wa kisheria
- Wakati wa mahojiano na IRCC au CBSA
- Kwenye kikao chako cha IRB-RPD
Ikiwa una wakili wa msaada, kliniki yake inaweza kulipia tafsiri kwa kiwango fulani. Ikiwa utaajiri wakili wa kibinafsi, itabidi ulipe ada hizo mwenyewe. Katika hali nyingine, kliniki za kusaidia watu kisheria bila malipo, rafiki yako, au mtu wa kujitolea anaweza kukusaidia na kukutafsiria.
Unaweza kuwa na mkalimani wa kitaalamu anaeongea lugha yako bila malipo kwenye kikao chako cha mkimbizi. IRB-RPD itachagua mkalimani atakae tumika, huwezi kuchagua wewe. Wakalimani wote wa IRB-RPD wamefunzwa na wana uzoefu wa kutafsiri mikutano ya kusikilizwa kwa wakimbizi.
Kile ambacho mkalimani wako anapaswa kufanya
Jukumu kuu la mkalimani ni kuhakikisha kila mtu anaweza kuelewana vizuri.
Wakalimani wanapaswa:
- Tafsiri kwa usahihi au kwa karibu iwezekanavyo. Hawapaswi kuongeza chochote au kuacha kitu chochote nje.
- Wasionyeshe kamwe ikiwa wanakubaliana au hawakubaliani na kitu chochote.
- Weka siri kila kitu kinachosemwa.
Mkalimani wako hatakiwi:
- Kukupa ushauri wa kisheria au kueleza mambo bila kwanza kupata ruhusa kutoka kwa anayezungumza.
- Kusema kile wanachofikiri ulimaanisha, au kufupisha au kufafanua unachosema.
Ikiwa unafikiri mkalimani amefanya makosa au ikiwa huelewi kitu, mwambie mwakilishi wako wa kisheria, Mwanachama, au afisa.
