Pata Mwakilishi wa Kisheria

Jua jinsi ya kupata mwakilishi wa kisheria. Elewa wanachofanya na unachopaswa kufanya. Jifunze jinsi ya kupata usaidizi ikiwa unafikiri kuwa hawafanyi kazi nzuri.

Pata Mwakilishi wa Kisheria

Mchakato wa kudai ukimbizi ni mgumu. Ni wazo zuri kuwa na mwakilishi wa kisheria akuongoze katika mchakato wa kudai ukimbizi. Huhitajiki kuwa na mwakilishi wa kisheria, lakini anaweza kukusaidia kufanya vizuri uwezavyo. Mwakilishi wa kisheria anaweza kukusaidia kuwasilisha dai lako, kuandaa ushahidi wako na kukusaidia katika kusikilizwa kwako.

Nani anaweza kuniwakilisha?

Watu hawa wanaweza kukuwakilisha (kutenda kwa niaba yako) wakati wa dai lako la ukimbizi:

  • Wakili
  • Mshauri wa uhamiaji
  • Mthibitishaji wa umma (ndani ya Quebec)
  • Msaidizi wa kisheria aliye na leseni (ndani ya Ontario)

Chagua mwakilishi wako wa kisheria kwa uangalifu. Je, atakusikiliza kwa makini? Je, atatenga muda kwa ajili yako? Je, yeye hujitokeza kila mara? Je, ni waaminifu? Je, anatoza kiasi sahihi cha fedha? Ikiwa huna uhakika, muulize wakala wa kusaidia wageni nchini anayeaminika kumhusu.

Vyama vya Sheria na Mashirika ya Kitaalam

Unataka kuamini kuwa mwakilishi wako wa kisheria anakuongoza vyema na kukupa ushauri mzuri. Hakikisha kuwa awe ni mwanachama wa shirika lao la kitaaluma.

Hii hapa tovuti ya chama cha sheria katika jimbo lako:

Ukiajiri mshauri wa uhamiaji, hakikisha kuwa yeye ni mwanachama wa Chuo cha Washauri wa Uhamiaji na Uraia. Washauri wa uhamiaji lazima waidhinishwe kabla ya kufanya kazi mbele ya IRB. Unaweza kuangalia Rejista ya Umma ili kuthibitisha hali ya mshauri wa uhamiaji.

Ukiajiri mwanasheria huko Ontario, angalia rekodi zao na Chama cha Wanasheria cha Ontario.

Ikiwa utaajiri mthibitishaji huko Quebec, angalia rekodi zake kwenye Chama cha wathibitishaji cha Québec.

Mwakilishi bila bure

Unaruhusiwa kuwa na mtu unayemwamini (kama vile mwanafamilia au rafiki) akupe usaidizi bila malipo kwenye dai lako. Mtu huyu anaitwa “mwakilishi bila ada.” Lakini ni bora ujaribu kupata mwakilishi wa kisheria.

Kufanya kazi na Mwakilishi wako wa Kisheria

Kuchagua mwakilishi wa kisheria ni muhimu sana. Jifunze jinsi mwakilishi wako wa kisheria anapaswa kufanya kazi nawe, nini hafai kufanya, na jukumu lako ni nini. Jua ni nini cha kufanya ikiwa unafikiri mwakilishi wako hafanyi kazi nzuri.

Jukumu lako kama mteja

Hata kama una mwakilishi wa kisheria, hili bado ni dai LAKO. Jukumu lako kama mteja ni:

  • Mpe mwakilishi wako wa kisheria ushahidi na hati zote atakazoitisha pamoja na taarifa yoyote mpya uliyo nayo. Usitume chochote kwa IRB-RPD bila kuzungumza na mwakilishi wako kwanza.
  • Mjulishe habari yoyote muhimu kuhusu nchi yako
  • Pokea simu zake na usome na ujibu barua zake pepe
  • Soma nyaraka au taarifa zozote watakazokupa.
  • Mpe hati au barua zozote utakazopata kutoka IRCC, CBSA au IRB-RPD.
  • Hakikisha kuwa anajua maelezo yako sahihi ya mawasiliano na mahali pa kuacha ujumbe.
  • Omba msaada unapohitaji.
  • Zungumza kuhusu vitu usivyokubaliana navyo.
  • Kuwa mkweli ili waweze kukusaidia vizuri iwezekanavyo.
  • Weka hati zako kwa mpangilio na uzingatie kazi zozote unazoambiwa ufanye.
  • Usichelewe kuhudhuria mikutano na vikao vyovyote.

Kujiwakilisha mwenyewe

Ikiwa huwezi kupata mwakilishi wa aina yoyote, lazima ujifanyie fomu yako ya BOC, na uende kwenye kikao chako.

Ikiwa huna msaada wa kisheria:

Fanya kazi na Mkalimani wako

Ikiwa huna uzoefu wa kuzungumza kwa Kiingereza au Kifaransa unaweza kuhitaji mkalimani wa kukusaidia kuwasiliana wa watu. Ni muhimu kuwa na mkalimani ili uelewe kile kinachotokea wakati wa dai lako la ukimbizi. Baadhi ya mifano ya wakati unaweza kuhitaji mkalimani ni:

  • Wakati unakutana na mwakilishi wako wa kisheria
  • Wakati wa mahojiano na IRCC au CBSA
  • Kwenye kikao chako cha IRB-RPD

Ikiwa una wakili wa msaada, kliniki yake inaweza kulipia tafsiri kwa kiwango fulani. Ikiwa utaajiri wakili wa kibinafsi, itabidi ulipe ada hizo mwenyewe. Katika hali nyingine, kliniki za kusaidia watu kisheria bila malipo, rafiki yako, au mtu wa kujitolea anaweza kukusaidia na kukutafsiria.

Unaweza kuwa na mkalimani wa kitaalamu anaeongea lugha yako bila malipo kwenye kikao chako cha mkimbizi. IRB-RPD itachagua mkalimani atakae tumika, huwezi kuchagua wewe. Wakalimani wote wa IRB-RPD wamefunzwa na wana uzoefu wa kutafsiri mikutano ya kusikilizwa kwa wakimbizi.

Kile ambacho mkalimani wako anapaswa kufanya

Jukumu kuu la mkalimani ni kuhakikisha kila mtu anaweza kuelewana vizuri.

Wakalimani wanapaswa:

  • Tafsiri kwa usahihi au kwa karibu iwezekanavyo. Hawapaswi kuongeza chochote au kuacha kitu chochote nje.
  • Wasionyeshe kamwe ikiwa wanakubaliana au hawakubaliani na kitu chochote.
  • Weka siri kila kitu kinachosemwa.

Mkalimani wako hatakiwi: 

  • Kukupa ushauri wa kisheria au kueleza mambo bila kwanza kupata ruhusa kutoka kwa anayezungumza.
  • Kusema kile wanachofikiri ulimaanisha, au kufupisha au kufafanua unachosema.

Ikiwa unafikiri mkalimani amefanya makosa au ikiwa huelewi kitu, mwambie mwakilishi wako wa kisheria, Mwanachama, au afisa.