Ukifika kwenye mpaka rasmi wa kuingia Kanada, unaweza kuanza dai la ukimbizi kwa Wakala wa Huduma za Mipaka ya Kanada (CBSA).
- Uwanja wa ndege wa kimataifa
- Mpaka rasmi wa kuvukia wa nchi kavu
- Bandari ya bahari
Mwambie afisa wa CBSA utakayekutana naye kwamba unataka kufanya dai la ukimbizi. Wataanza mchakato huo na wewe.
Elewa mchakato wa kufanya dai la ukimbizi mpakani
Mara tu unapomwambia afisa wa CBSA kwamba unataka kufanya dai la ukimbizi, anaweza kukuuliza maswali ili kuamua kama dai lako linastahili kuwasilishwa kwa IRB-RPD.
Kwa kawaida pia watajaza fomu za madai ya ukimbizi pamoja nawe, watachukua hati zako za kitambulisho na/au pasipoti, na kuchukua alama za vidole na picha yako (bayometriki).
Iwapo afisa wa CBSA ataamua kuwa unastahiki kufanya dai la ukimbizi atakupa:
- Hati ya Utambulisho ya Ulinzi wa Wakimbizi (RPID)
- Barua inayothibitisha kuwa dai lako la ukimbizi limetumwa kwa Kamati ya Uhamiaji na Wakimbizi ya Kanada (IRB)
- Maelekezo kuhusu jinsi na wakati wa kuwasilisha Fomu yako ya Msingi wa Madai (BOC)
- Maagizo kuhusu jinsi na wakati wa kufanya Uchunguzi wa Kiafya wa Uhamiaji (IME)
Iwapo afisa wa CBSA hatabaini kustahiki kwako, atakupa maagizo kuhusu kuhudhuria mahojiano ya ustahiki yatakayofanyika tarehe nyingine. Ikiwa hii itatokea, watakupa:
- Hati ya Kukiri Madai yako yamepokelewa
- Maagizo kuhusu jinsi na wakati wa kufanya Uchunguzi wa Kimatibabu wa Uhamiaji (IME)
- Maagizo kuhusu jinsi na wakati wa kujaza fomu zako za kudai ukimbizi – unaweza kuambiwa ujaze fomu hizi mtandaoni kupitia tovuti ya IRCC.
Baada ya kurejea na kufanya mahojiano ya kustahiki, ikiwa utapatikana kuwa unastahiki, utapokea Hati ya Utambulisho ya Ulinzi wa Wakimbizi, barua inayothibitisha kuwa dai lako la ukimbizi limetumwa kwa IRB, na maagizo ya kuwasilisha fomu yako ya BOC.
Kizuizini
CBSA inaweza kukuweka kizuizini (kukuweka chini ya ulinzi) ukifika katika mpaka wa Kanada. Hii inaweza kuwa kwa sababu CBSA:
- hawana uhakika wewe ni nani
- hawaamini kuwa utarudi baadaye kujibu maswali zaidi
- hawaamini kuwa unaweza kutoa dai la ukimbizi na wanataka kukuondoa nchini
- Wanaamini wewe ni mtu hatari
- waanajua wewe una rekodi ya uhalifu
Ikiwa umezuiliwa, wasiliana na mwakilishi wa kisheria ili upate kujua kama unaweza kuachiliwa. Unaweza kufuzu kupata wakili wa bure au wa bei nafuu kupitia kwa kliniki ya kusaidia watu kisheria. Pata maelezo zaidi kuhusu kuwekwa kizuizini hapa.
